Teknolojia Inayolea
Kila Nyota.

SMART. SIMPLE. SECURE.

Kikokotoo cha Biashara ya SMS

Makadirio ya gharama ya SMS kwa mwezi mmoja kulingana na idadi ya wanafunzi wako.

100 STUDENTS5,000 STUDENTS

100

Jumla ya Wanafunzi

TZS 10,500

Makisio ya Malipo / Mwezi (@ 35/=)

ElimuCloud Ecosystem

Mazingira kamili ya kidijitali yanayounganisha kila idara shuleni kwako.

Academic SIS Portal

Mfumo wa Academic SIS ndio mhimili mkuu wa taaluma katika shule ya kisasa. Moduli hii inaondoa adha ya walimu kutumia Excel au mahesabu ya mkono ambayo mara nyingi husababisha makosa ya kibinadamu. Kupitia SIS, mwalimu anaingiza alama mara moja tu, na mfumo unachakata kila kitu: kuanzia wastani wa masomo, GPA, Division, hadi nafasi (Rank) za wanafunzi darasani na ngazi ya shule nzima. Inazalisha ripoti fomu za kisasa zenye picha ya mwanafunzi, QR Code ya usalama, na uchambuzi wa kina wa maendeleo ya mwanafunzi tangu anapoanza shule hadi anapomaliza. Ni suluhisho la uhakika kwa shule za Msingi (Primary) na Sekondari (Secondary) zinazofuata viwango vya NECTA.

NECTA Terminal Reports
GPA & Division Auto-Calc
REQUEST SIS DEMO

Digital Lesson Plans

Moduli ya Digital Lesson Plans inalenga kuleta mapinduzi ya kijani (Paperless) shuleni kwa kuondoa hitaji la walimu kuandika maandalio ya masomo kwenye vitabu vizito kila siku. Sasa, walimu wanaweza kuandaa maandalio yao kidijitali kupitia simu, tablet, au laptop zao. Mfumo unakuja na templates tayari kulingana na mtaala wa TIE (Taasisi ya Elimu Tanzania). Faida kuu ni kwamba Mkuu wa Shule au HOS anaweza kupitia, kutoa maoni, na kuidhinisha (Approve) maandalio hayo popote alipo duniani kupitia dashibodi yake, hali inayoongeza uwajibikaji na ubora wa ufundishaji darasani.

Payments & EFD Hub

Usimamizi wa fedha ni eneo nyeti katika taasisi yoyote ya elimu. Payments & EFD Hub inaleta uwazi wa 100% katika mapato ya shule. Inaruhusu kurekodi ada za wanafunzi, michango ya chakula, na malipo mengine yote kwa mfumo wa kidijitali. Kila malipo yanapofanyika, mfumo unatoa risiti ya kielektroniki yenye QR Code ambayo mzazi anaipata papo hapo kupitia SMS au anaweza kuipakua. Moduli hii pia inasaidia ufuatiliaji wa wadaiwa (Debtors) na inazalisha ripoti za fedha (Profit & Loss) za kila siku, wiki, na mwezi, hali inayosaidia uongozi kufanya maamuzi sahihi ya kifedha.

Smart Attendance

Usalama wa mwanafunzi ni kipaumbele namba moja kwa kila mzazi. Moduli ya Attendance Hub inaruhusu shule kufuatilia mahudhurio kwa kutumia teknolojia ya kadi (Smart Cards) au manual entry. Mwanafunzi anapofika shuleni na kugusisha kadi yake, mfumo unamtumia mzazi SMS papo hapo kumtaarifu kuwa mtoto amefika salama. Vilevile, mwanafunzi asipofika shuleni baada ya muda fulani, mzazi anapata taarifa ya utoro. Pia, moduli hii inatunza kumbukumbu za nidhamu na adhabu alizopewa mwanafunzi kwa ajili ya marejeo ya baadae.

Smart SMS Gateway

Mawasiliano ndio daraja kati ya shule, walimu, na wazazi. Bulk SMS Gateway ya ElimuCloud ni chombo chenye nguvu kinachoweza kutuma maelfu ya ujumbe kwa sekunde chache. Shule inaweza kutumia mfumo huu kutangaza vikao vya wazazi, kutuma dharura, salamu za sikukuu, au matokeo ya mitihani kwa kila mzazi kwa jina lake. Mfumo wetu umetengenezwa kuwa wa gharama nafuu zaidi (35/= tu kwa kila unit) na unahakikisha ujumbe unafika kwa jina la shule yako (Custom Sender ID), jambo linaloongeza heshima na weledi wa taasisi yako.

Retail POS & Store

Shule nyingi zina maduka ya sare, vitabu, au vinywaji, lakini upotevu wa mali umekuwa changamoto. Moduli ya Retail POS inaruhusu kusimamia mauzo yote ya duka la shule kidijitali. Inadhibiti 'Inventory' kwa kuonyesha kiwango cha bidhaa kilichobaki ghalani (Store) na kutoa taarifa pale bidhaa zinapokaribia kuisha. Pia, inarekodi matumizi (Expenses) yote ya shule ya kila siku, kuanzia ununuzi wa chaki hadi matengenezo ya magari, ili kutoa picha kamili ya matumizi ya taasisi.

Staff HR & Payroll

Wafanyakazi ndio injini ya shule. Moduli ya HR & Payroll inasaidia kusimamia mafaili ya walimu na wafanyakazi wasio walimu, mikataba yao ya kazi, na taarifa za kitaaluma. Sehemu ya Payroll inarahisisha ukokotoaji wa mishahara kila mwezi, ikijumuisha makato ya kisheria (NSSF, PSSSF, PAYE) na mikopo ya wafanyakazi. Inazalisha 'Payslips' za kisasa na ripoti za malipo kwa ajili ya benki, hali inayopunguza muda mwingi unaotumiwa na muasibu au mkuu wa shule kila mwisho wa mwezi.

Transport System

Kusimamia mabasi ya shule ni kazi kubwa inayohitaji umakini. Moduli hii inasaidia kupangilia njia (Routes) ambazo kila basi linapita na orodha ya wanafunzi wanaopaswa kupanda basi hilo. Pia, inarekodi matumizi ya mafuta, matengenezo ya magari (Maintenance), na tarehe za bima au leseni zinapokaribia kuisha. Inasaidia pia kurekodi muda ambao basi limeondoka shuleni na kurudi, jambo linalohakikisha usalama wa wanafunzi na nidhamu ya madereva.

E-Learning Hub

ElimuCloud haishui tu utawala, bali pia inaboresha ujifunzaji. E-Learning Hub inaruhusu walimu kupakia (Upload) miongozo ya masomo (Notes), video za mafunzo, na mitihani ya mazoezi kwa ajili ya wanafunzi. Wanafunzi wanaweza kupata maudhui haya wakiwa nyumbani kupitia akaunti zao, jambo linalofanya ujifunzaji uendelee hata nje ya saa za shule. Ni chombo bora cha kusaidia wanafunzi wanaohitaji marudio ya ziada au wakati wa dharura ambapo shule zimefungwa.

Financial Insights

Kwa mmiliki wa shule au uongozi wa juu, kupata picha ya jumla ya hali ya shule ni muhimu. Moduli ya Financial Insights inakusanya data kutoka moduli zote na kuzionyesha katika mfumo wa grafu na chati rahisi kueleweka. Unaweza kuona mlinganisho wa mapato na matumizi, kasi ya ulipaji wa ada, na maeneo yanayotumia fedha nyingi zaidi. Hii inakupa 'Power' ya kudhibiti bajeti ya shule yako kwa weledi na kuzuia uvujaji wa mapato usio wa lazima.

Academic SIS
150,000/= Yearly
TAARIFA ZAIDI →
Lesson Plans
100,000/= Yearly
TAARIFA ZAIDI →
Payments Hub
Integrated
TAARIFA ZAIDI →
Attendance
50,000/= Yearly
TAARIFA ZAIDI →
Smart SMS
35/= Per Unit
TAARIFA ZAIDI →
Starter Pack
Small School
TAARIFA ZAIDI →
Retail POS
Store Module
TAARIFA ZAIDI →
Staff HR
Payroll Ready
TAARIFA ZAIDI →

Video Demos

Testing link
Kutazama matokeo